logo

MSIWE VYANZO VYA KUSABABISHA MIGOGORO-DKT. RWEZIMULA

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt .Franklin Rwezimula amewataka wasaidizi wa kisheria wawe mabalozi wa kuimarisha haki na wasiwe vyanzo vya kusababisha migogoro bali wawe ni watatuzi wa migogoro kwa jamii .

Dkt.Rwezimula ametoa rai hiyo leo Februari 26,2025 wakati akifungua mafunzo ya siku 15 kwa wasaidizi wa msaada wa kisheria ambapo amesema jumla ya washiriki 42 watapewa mafunzo hayo kutoka mikoa ya Dodoma ,Tanga na Singida .

Amesema jukumu kubwa la wasaidizi wa kisheria ni kujenga uwezo kwa jamii katika kutambua na kusimamia haki na wajibu wao kwa kufanya hivyo kutakuwa na jamii yenye upendo,amani na utulivu kwani kila mmoja atalinda na kuhifadhi haki za wengine na hivyo kupunguza utendaji wa makosa .

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa LSF Amani Manyelezi amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajemgea uwezo watoa msaada wa kisheria ili kiwasaidia kuwa na uwezo wa kitoa Msaada wa Kisheria kwenye ngazi walizopo.

“Kazi yao kubuwa ni kuhakikisha kwamba wanashughulika na mashauri mengi kabla hajaenda mahakamani na tinajua wanafamya kazi kubwa kutatua migogoro ya watu na kuwasaidia wananchi kujua haki zao za msingi” alisema.

Nao Monica Jacob na Juma Waziri washiriki wa mafunzo hayo wamesema watanarajia kuwa mabalozi wa masuala ya uelewa wa kisheria na watajikita katika kutatua migogoro inayotokea katika maeneo yao.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn