logo

BMH YAPOKEA VITIMWENDO 30 KUTOKA KWA MDAU WA AFYA

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imepokea viti mwendo 30 na medical oxygen concentrators 4 vyenye thamani ya shilingi milioni 28 kutoka kwa mdau wa Afya kutoka Dar es Salaam.

Akipokea msaada huo, Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Prof.Abel Makubi, ameahidi msaada utatumika kwa wagonjwa kama ilivyokusudiwa.

"Leo, tumepata mdau kutoka Dar es Salaam ambaye amekuja kutuunga mkono. Tunaahidi misaada hii itatumika kama ilivyokusudiwa kwa wagonjwa," amesema Mkurugenzi Mtendaji.

Kwa upande wake, mdau wa Afya huyo, Mzee Akhter Khakoo, amesema ametoa msaada huo kwa kushirikiana na familia yake.

"Bado nitaendelea kutoa misaada kama hii kwa Hospitali za umma, Nathan kwa kushirikiana na familia yangu," amesema Mzee Khakoo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn