logo

UKUAJI SEKTA YA MADINI UMEONGEZEKA KUTOKA ASILIMIA 9.4 HADI KUFIKIA ASILIMIA 11.3 -MHANDISI LWAMO

Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Ramadhani M. Lwamo, amesema ukuaji wa sekta ya madini umeongezeka kutoka asilimia 9.4 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 11.3 mwaka 2023.

.

Lwamo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa tume hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita leo tarehe 4 Machi, 2025, katika ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, Dodoma.

.

Amesema Tume imefanikiwa kutoa jumla ya leseni 41,424 kati ya 37,318 zilizopangwa kutolewa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo ni sawa na asilimia 111.

"Leseni hizo zilijumuisha leseni za uchimbaji mkubwa, uchimbaji wa kati na uchimbaji mdogo" alisema.

.

Amesema Mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 7.2 mwaka 2021 hadi asilimia 9 mwaka 2023 kutokana na kuimarika kwa usimamizi wa shughuli mbalimbali za madini.

.

"Kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 mauzo ya madini katika masoko na vituo vya ununuzi wa madini yameendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 2.361.80 hadi shilingi bilioni 2,597.18 kwa mwaka 2023/2024" alisema Lwamo.

.

Aidha, Lwamo amesema Tume imefanikiwa kutenga maeneo 58 kwa ajili ya wachimbaji wadogo katika mikoa mbalimbali.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn