DUWASA WAIPAMBA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI JIJINI DODOMA
Wanawake wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) wameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa Mkoa wa Dodoma katika uwanja wa Chinangali Park.
Maadhimisho hayo kimkoa yalihudhuriwa na wanawake kutoka katika Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma akiwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Alhaj Jabir Shekimweri.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA, Mhandisi Aron Joseph amesema inapoadhimishwa kilele cha Siku ya Wanawake Duniani anatambua kuwapongeza wanawake wote wa DUWASA kwa uwezo wao mkubwa katika utendaji kazi.
“Ni dhahili mmekuwa kiungo na nguzo imara ya Taasisi yetu kusonga mbele kwa mafanikio makubwa" Alisema Mhandisi Aron.
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa yamefanyika katika Mkoa wa Arusha ambayo kauli mbiu kwa mwaka huu ni “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji.”
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

