logo

DKT.MPANGO AWATAKA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJENGA KWENYE SHOROBA ZA WANYAMA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewataka Wananchi Wanaoishi karibu Na Hifadhi za Wanyama Kuacha tabia ya kujenga kwenye shoroba za Wanyama na kung’ang’ania kuvamia hifadhi badala yake waondoke kupisha hifadhi kwa kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na maeneo mengi ambayo yanafaa kwa kuishi kama ambavyo baadhi ya wananchi wa Ngorongoro walivyoamua kwa hiari yao kuondoka kwenda kuishi Msomela Tanga kupisha uhifadhi.

.

Mpango Ameyasema Hayo Mei 16, 2023 Alipokuwa Karatu mkoani Arusha wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa ofisi ya Makao makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kwenye ufunguzi wa Hospitali ya Karatu.

.

Makamu Huyo Pia amesisitiza wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo ya Hifadhi na kushirikiana na majangili katika kuvunja sheria baadala yake washirikiane na wahifadhi ili kutunza maliasili kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye.

.

"Ndugu zangu nawasihi sana tutunze mazingira yetu, tusipotunza tunakuwa tunajiangamiza wenyewe” Alisema Mpango.

.

Mpango Ametoa wito kwa viongozi wa dini, vyama vya siasa na wabunge kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi Kwa Wananchi.

Katika hatua nyingine, Mpango ameielekeza Wizara ya maliasili na Utalii kushirikiana na vyuo vikuu vya hapa nchini kufanya utafiti wa kina kuhusu mimea vamizi kwenye hifadhi ili kufa na suluhisho la changamoto hiyo.

Akimkaribisha Makamu wa Rais kutoa hotuba yake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mohamed Mchengerwa amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia na kutoa fedha za kufanyika kwa ujenzi huo.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn