DUWASA YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM SHULE YA MSINGI MKOKA JIJINI DODOMA
WANAWAKE kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) leo Machi 10, 2025 wametoa mahitaji yenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kwa watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya Msingi Mkoka iliyopo Wilaya ya Kongwa jijini Dodoma.
Akizungumza katika shule hiyo yenye wanafunzi wenye mahitaji maalum, Katibu wa wanawake wa DUWASA, Ester Mlewa amesema ni utaratibu wa DUWASA kila mwaka hususani katika Maadhimisho ya siku ya Wanawake kuwatembelea watu wenye mahitaji maalum kuonesha upendo.
Naye, Mwalimu wa Kitengo cha watoto wenye mahitaji maalum katika shule hiyo, Furaha Mwashilindi ameishukuru DUWASA kwa kujitoa kuwasaidia wanafunzi hao mahitaji mbalimbali.
Aidha, amesema shule hiyo yenye wanafunzi 122 inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu ambapo kwa sasa wapo watano na vifaa vya ujifunzaji na ufundishaji.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

