WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHIRIKI JUBILEI YA MIAKA 25 YA UASKOFU WA ASKOFU KILAINI
WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa amesema jamii inahitaji kufundishwa, kutambua na kuenzi mila za Kitanzania, pamoja na kujiepusha na vishawishi vya kuiga tabia za kigeni ambazo hazina manufaa kwa ustawi wa Taifa.
Mheshimiwa Majaliwa ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Machi 19, 2025) katika Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Msaidizi Mstaafu wa Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki Bukoba Askofu Method Kilaini.
“Sote tumekua tukishuhudia ongezeko la vitendo vya ukosefu wa maadili katika jamii. Vitendo hivi vinatokana na malezi hafifu lakini pia watu kuiga mila na desturi kutoka mataifa mengine ambazo haziendani na tamaduni na maadili yetu ya Kitanzania.” alisema.
Waziri Mkuu amesema hali hiyo imeathiri mwenendo wa jamii, hususan kwa vijana ambapo wanashuhudia mabadiliko katika misingi ya familia, jamii, na Taifa kwa ujumla.
.
Amesema Kanisa lina nafasi ya pekee katika kuhakikisha Taifa linarudisha maadili ya kweli ya Kitanzania yanayofundisha kuheshimu utu, haki, na amani.
.
“Serikali, tunatambua mchango mkubwa wa Kanisa katika hili na tutashirikiana nalo ili kuleta mabadiliko chanya kwa kizazi cha sasa na kijacho.” alisema.
Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa madhebu ya dini ikiwemo Kanisa Katoliki katika kuboresha ustawi wa jamii.amii yetu,hivyo amewaomba viongozi wa dini nchini waendelee kuwa nguzo ya maadili bora, kwa kutoa mwongozo wa kiroho na kijamii.
Akizungumza kuhusu Askofu Kilaini, Mheshimiwa Majaliwa amesema ni kielelezo cha ujasiri, imani thabiti, na huduma ya kujitolea kwa Kanisa na jamii ya Watanzania, ameonesha nguvu ya uvumilivu, akiwa na michango mikubwa katika maisha ya kanisa.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

