logo

RAPA TAY-K AHUKUMIWA MIAKA 80 JELA KWA KUMPIGA RISASI MPIGA PIGA SALDIVAR TEXAS MAREKANI

Rapa kutoka nchini Marekani, Tay-K amehukumiwa kifungo cha miaka 80 jela kwa kosa la mauaji ya mpiga picha Mark Anthony Saldivar mwaka 2017 huko Texas.

Taymor McIntyre, anayejulikana kama Tay-K 47, amepatikana na hatia hiyo mapema wiki hii ya mauaji hayo.

.

Baraza la majaji Kaunti ya Bexar, Texas, limetoa hukumu yake jana jumanne April 15,2024 baada ya saa nyingi za ushahidi wakati wa awamu ya adhabu ya kesi hiyo.

Kwa sasa Tay-K yuko rumande katika Idara ya Haki ya Jinai ya Texas, ambapo ataendelea kuzuiliwa.

.

Rapa huyo alikuwa anakabiliwa na kifungo cha maisha jela na uwezekano wa kuachiliwa huru.

.

Hukumu hiyo inajiri baada ya Tay-K kupatikana na hatia siku ya Jumatatu ya mauaji yaliyotokana na kumpiga risasi Saldivar mwaka wa 2017.

.

Kulingana na waendesha mashtaka, kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye alikuwa na umri wa miaka 16 wakati huo, alimpiga risasi na kumuua Saldivar baada ya kuiba vifaa vyake vya kupiga picha.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn