logo

MAKUSANYO YA FEDHA ZA MFUKO WA BARABARA MWAKA WA FEDHA 2024/25 YAMEFIKIA SHILINGI BILIONI 905.2

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema Serikali imefanikiwa kuongeza makusanyo ya mfuko wa Barabara kutoka shilingi Bilioni 899.2 mwaka 2020/21 hadi shilingi Bilioni 1,113.3 mwaka wa fedha 2023/24 sawa na ongezeko la asilimia 24.

.

Aidha, Amesema hadi mwezi April,2025 makusanyo ya fedha za mfuko kwa mwaka wa fedha 2024/25 yalikuwa yamefikia shilingi Bilioni 905.2.

.

"Ongezeko hilo limewezesha kuimarika kwa uwezo wa mfuko kugharamia matengenezo ya Barabara nchini" amesema.

Mhe. Ulega ameyasema hayo leo tarehe 05 Mei,2025 alipokuwa akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 Bungeni jijini Dodoma.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn