MIRADI 68 YENYE UWEZO WA KUHUDUMIA WANANCHI 3,362,850 IMEKAMILIKA -WAZIRI AWESO
"Hadi mwezi Aprili 2025, Wizara imeendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya mijini ambapo miradi 68 yenye uwezo wa kuhudumia wananchi 3,362,850 imekamilika.
.
"Baadhi ya miradi iliyokamilika ni pamoja na Mradi wa ujenzi wa mtandao wa usambazaji maji na matanki ya kuhifadhia maji Kusini mwa Dar es Salaam unaohudumia wananchi wapatao 450,000 wa maeneo ya Bangulo, Mwanagati, Kitunda, Kipunguni, Majohe, Kivule, Magole, Msongola, Chanika, Chalambe, Kinyerezi na Kifuru; Mradi wa Maji Mugango-Kiabakari-Butiama unaohudumia zaidi ya wananchi 100,000; na Mradi wa Maji Same-Mwanga- Korogwe uliozinduliwa rasmi na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 9 Machi, 2025 na unahudumia wananchi wapatao 456,900" alisema Aweso.
.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameyasema hayo leo Mei 08,2025 alipokuwa akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka wa Fedha 2025/2026 Bungeni jijini Dodoma.
.
Aidha, Waziri Aweso amesema kuna miradi 226 inayoendelea na utekelezaji katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mradi wa kuboresha huduma ya maji katika Jiji la Mbeya kwa kutumia chanzo cha Mto Kiwira; Mradi wa kuboresha huduma ya majisafi katika Jiji la Dodoma kwa maeneo ya Nzuguni, Ilazo, Swaswa na Chamwino; Mradi wa kuboresha huduma ya maji katika Jiji la Mwanza maeneo ya Kisesa, Buswelu, Luchelele pamoja na Wilaya za Ilemela, Magu na Misungwi; Mradi wa kuboresha huduma ya maji katika Manispaa ya Morogoro utakaonufaisha wananchi wa maeneo ya Mindu, Mikoroshini, Mkwajuni, Madaganya, Kingolwira, Misongeni, Kitungwa, Kihonda na Mkundi; Mradi wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika Mkoa wa Simiyu utakaonufaisha wananchi wa Wilaya za Bariadi, Busega, Itilima, Meatu na Maswa wenye zaidi ya Bilioni 400; Mradi wa Bwawa la Kidunda kwa kutumia fedha za ndani jumla ya Bilioni 329; na Mradi wa kuboresha huduma ya maji katika miji 28 ya: Handeni, Korogwe, Muheza, Pangani, Kilwa-Masoko, Nanyumbu, Ifakara, Rujewa, Chunya, Njombe, Makambako, Wanging’ombe, Kiomboi, Singida, Manyoni, Mugumu, Chemba, Chamwino, Kasulu, Mpanda, Sikonge, Urambo, Kaliua, Kayanga, Chato, Geita.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

