WIZARA YA MAJI KUFUATILIA UBORA WA MAJI KATIKA VYANZO VYA MAJI 2,200 -WAZIRI AWESO
Wizara ya Maji imepanga kuendelea kuhakiki na kufuatilia ubora wa maji katika vyanzo vya maji 2,200; mifumo 8,245 ya usambazaji maji katika maeneo ya vijijini na mijini; na mifumo 150 ya ubora wa majitaka kwa mwaka 2025/26.
.
Aidha, Wizara hiyo itaendelea kuhakiki na kufuatilia ubora wa madawa yanayotumika kusafisha na kutibu maji katika mamlaka za maji, pamoja na CBWSOs.
.
Vilevile, Wizara imepanga kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na utunzaji wa takwimu na taarifa za ubora wa maji, sambamba na kuwezesha uandaaji na ufuatiliaji wa utekelezaji wa mipango ya usalama wa maji katika mamlaka za maji 40 na CBWSOs 120.
Pia, Wizara imepanga kuanza ujenzi wa majengo ya maabara za Arusha na Tanga; na kuzipatia maabara za maji vitendea kazi pamoja na kuziwezesha kupata na kudumisha ithibati ya viwango vya kimataifa.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

