MIKATABA ZAIDI YA LAKI MOJA IMETOLEWA KWA WAZABUNI KUPITIA NeST- BW.SIMBA
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Dennis Simba amesema mikataba 130,032 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Trilioni 14.9 imetolewa kwa wazabuni kupitia Mfumo wa NeST kwa uwazi na haki tangu Julai 1,2023, hatua ambayo imeongeza ajira na kukuza Uchumi wa watanzania wengi.
Ameyasema hayo leo, Mei 12, 2025 akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio ya Mamlaka hiyo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameongoza kuwa katika kipindi hiki, makundi maalum (wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu) yamepata zabuni zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 15 kupitia Mfumo wa NeST,hatua inayoongeza ushirikishwaji wa wananchi wa matabaka yote katika kujenga Uchumi.
Aidha, Bw. Simba amesema kuwa kwa kuzingatia ufanisi wa Mfumo wa NeST na uchunguzi uliofanywa na Mamlaka hiyo, imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 17.52.
.
Mafanikio mengine aliyoyaeleza ni pamoja na kusaidia kuhakikisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT) ya Shilingi milioni 289.76 inakusanywa.
.
Aidha, amesema Mamlaka hiyo imesaidia kubaini madai batili ya wazabuni ya Shilingi bilioni 1.68 na kupitia ufuatiliaji imesaidia kufanya marekebisho ya mikataba yenye tofauti ya shilingi Bilioni 14.65.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

