BMH YAONDOA UVIMBE MKUBWA KWENYE UBONGO WENYE UKUBWA WA PARACHICHI
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) imefanikiwa kuondoa uvimbe mkubwa wa ubongo kwa mwanamke mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Mtumba, jijini Dodoma.
Daktari Bingwa wa ubongo na mishipa ya fahamu, Maxgama Ndosi, aliyeongoza upasuaji huo, amesema kuwa uvimbe uliokuwa upande wa kulia wa ubongo wa mgonjwa ulikuwa na ukubwa wa tunda la parachichi.
"Alikuja akiwa hawezi kutembea baada ya uchunguzi wa kitabibu tukagundua ana uvimbe mkubwa kwenye ubungo ambao ulihitaji upasuaji wa haraka ili kumuokoa," alisema Dkt. Msosi.
Bi Olivier Udoba, ambaye ni mama mzazi wa mgonjwa huyo, ameishukuru Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa huduma hiyo ya matibabu.
.
Aidha, Bi.Udoba amesema kuwa binti yake alianza kuumwa toka mwaka jana mwezi wa Septemba na kwamba alikuwa akipata changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo kupata degedege.
"Mwanzoni tulikuwa tumepanga kumpeleka Dar es Salaam hivyo tulivyoona hali yake inazidi kuwa mbaya tukabadili maamuzi tumlete hapa Hospitali ya Benjamin Mkapa," alisema.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

