logo

WIZARA YA KILIMO YALIOMBA BUNGE KUIDHINISHA BAJETI YA TRILIONI 1.24 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

Wizara ya Kilimo imeliomba Bunge liidhinishe jumla ya kiasi cha Shilingi 1,242,975,075,000 katika mwaka 2025/2026 ili kuendelea kutekeleza miradi mbalimbali ambayo inalenga kuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kwa upande wa mazao kufikia asilimia 5 na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kimkakati.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2025/2026 tarehe 21 Mei 2025, Bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) ameeleza kuwa Wizara itaendelea kutekeleza vipaumbele sita (6) kwa kuendelea na utekelezaji wa miradi iliyoanza mwaka 2022/2023, 2023/2024 na 2024/2025 na kuanza miradi mipya.

“Miradi hiyo inajumuisha miradi ya umwagiliaji, vituo vya zana za kilimo, upatikanaji wa pembejeo za kilimo, uhifadhi, uongezaji thamani, uanzishaji wa mashamba makubwa ya pamoja, uzalishaji, ujenzi wa masoko, utafiti, huduma za ugani na utoaji wa ruzuku ya pembejeo za kilimo.” amesema Mhe. Hussein Bashe.

Ameongeza kuwa malengo hayo yatafikiwa kwa kutekeleza vipaumbele ambavyo ni kuongeza tija na uzalishaji; kuchangia kuongeza ajira zenye staha na ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo; kuimarisha usalama wa chakula na lishe, kuimarisha upatikanaji wa masoko, mitaji na mauzo ya mazao nje ya nchi; kuimarisha maendeleo ya ushirika pamoja na kuimarisha matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika uendelezaji wa Sekta ya Kilimo

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn