UZALISHAJI WA KOROSHO UMEONGEZEKA HADI TANI 528,263.82-WAZIRI BASHE
"Uzalishaji wa mazao asilia ya biashara umeongezeka kutoka tani 898,967 mwaka 2020/2021 hadi tani 1,451,694.11 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 61.5" alisema Bashe.
.
Waziri Bashe ameyasema hayo leo Mei 21,2025 alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa fedha wa 2025/26 Bungeni jijini Dodoma.
.
Bashe amesema uzalishaji wa korosho umeongezeka kutoka tani 210,786 msimu wa 2020/2021 hadi tani 528,263.82 msimu wa 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 150.61.
.
Aidha, Waziri Bashe amesema uzalishaji wa tumbaku umeongezeka kutoka tani 58,508 msimu wa 2020/ 2021 hadi tani 160,000 msimu wa 2024/2025 sawa na ongezeko la asilimia 173.47 na kuifanya Tanzania kuwa mzalishaji wa pili Afrika.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

