WANAFUNZI ZAIDI YA 200,000 KUSHIRIKI MASHINDANO YA NBC YA UANDISHI WA INSHA NA WAZO BUNIFU LA BIASHARA TANZANIA
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, leo Mei 24, 2025 Jijini Dar es Salaam amezindua rasmi Mashindano ya NBC Essay Writing and Business Idea 2025, yanayolenga kukuza umahiri wa uandishi, ubunifu wa kibiashara na elimu ya kifedha miongoni mwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini.
Waziri Mkenda amesema kuwa mashindano hayo ni jukwaa la kitaifa la kuamsha fikra za ubunifu na kuchochea ndoto kwa vijana wa Kitanzania watakaoliongoza Taifa kwa maarifa, weledi na ubunifu.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuwashirikisha zaidi ya wanafunzi 200,000 kutoka shule za sekondari za umma na binafsi nchi nzima.
Maeneo yanayoshindaniwa ni pamoja na Uandishi wa Insha na Wazo Bunifu la Biashara.
Aidha, ameisifu hatua ya Benki hiyo kuwekeza katika elimu ambapo amesema yanachochea maendeleo chanya.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wa Benki ya NBC, wadau wa elimu, waalimu, wazazi na wanafunzi.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

