logo

RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA OFISI ZA CCM MAKAO MAKUU DODOMA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Mei 28, 2025 akiwa pamoja na viongozi wengine, ameweka Jiwe la Msingi la Jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jijini Dodoma.

Rais Samia amesema tukio hili muhimu ni hatua nyingine inayoakisi ndoto za waasisi wetu na wananchi kwa ujumla, juu ya kuanzishwa kwa CCM.

.

"Lengo la waasisi wetu, wanachama na kila Mtanzania ni kuiona CCM inayoendelea kuwa jukwaa la wananchi kuamua hatma yao, na kudumu kuwa madhubuti katika kupanga na kutenda kwa manufaa ya wananchi" alisema Rais Samia.

Aidha, Amesema wataendelea kuboresha miundombinu si tu katika Makao Makuu hayo mapya ya CCM, bali pia kwenye ofisi za chama nchi nzima.

.

"Chama hiki ni mali ya wananchi. Ofisi hizi zitatumika si tu kwa shughuli za chama na utawala, bali pia kama sehemu ya kuwaandaa vijana kujijenga kiuongozi na kimaadili kupitia mafunzo, tafiti, sera, itikadi na mijadala kwa mustakabali wa Taifa letu" alisema Rais Samia.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn