BANZI AHUDHURIA SEMINA YA UWEKEZAJI ILIYOANDALIWA NCHINI JAPAN
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT), Bi. Beatrice Banzi amehudhuria semina ya uwekezaji iliyoandaliwa na Shirika na Maendeleo ya Viwanda la Umoja wa Mataifa(UNIDO) iliyofanyika Jijini Tokyo nchini Japan.
Semina hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Japan yaani Japan Expo yanayoendelea nchini humo.
.
Wadau mbalimbali wakiwemo kutoka hapa nchini wameshiriki semina hiyo.
Akiwa kwenye semina hiyo Mkurugenzi Beatrice alikutana na kuzungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
hapa nchini, Shigeki Komatsubara ambapo alitumia wasaha huo kujadiliana namna ya kuendesha Sekta ya Chai hususan kwa kuwasaidia wakulima wadogo wa chai wa hapa nchini.
“Hii imekuwa ni fursa adhimu kushiriki kwenye semina hii muhimu ambapo pamoja na mambo mengine Bodi ya Chai imekutana na mdau huyu mkubwa pamoja na wadau wengine wa maendeleo na hakika mwanga kwenye sekta ya chai unazidi kuonekana ambapo kama nchi itarajie makubwa zaidi.” alisema Mkurugenzi Beatrice.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

