MAWAKILI VIJANA WAASWA KUJIFUNZA ZAIDI ILI KUTAMBUA HAKI ZA BINADAMU
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa amewasihi Mawakili wote nchini (hususani vijana) wapende kujifunza zaidi ili waweze kutambua haki za binadamu.
.
Ole Ngurumwa ameyasema hayo Juni 28,2025 alipokuwa akifungua Mafunzo ya siku mbili (2) ya Elimu ya Sheria kwa Wanasheria wa Haki za Binadamu nchini Tanzania yanayofanyika Jijini Dodoma.
.
Aidha, Wakili Ole Ngurumwa ameishauri Serikali ya kwamba tunapokwenda kwenye uchaguzi wa mwaka huu 2025, uchaguzi uwe wa uhuru na haki ili wabunge wa upinzani waingie bungeni ili tuweze kupata kambi ya upinzani.
.
"Tunapokuwa na kambi ya upinzani bungeni, ule ubora wa Bunge utaimarika zaidi" alisema Ole Ngurumwa.
.
Mafunzo hayo yamewakutanisha wanasheria na mawakili zaidi ya 50 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

