SHULE 137 MPYA ZIMEJENGWA KATAVI NDANI YA MIAKA 4 YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA
Mkoa wa Katavi ni Moja ya Mkoa ambao unakua kwa kasi, kati ya Mikoa michache iliyoanzishwa hivi karibuni, huku ikishika nafasi ya tano kwenye uzalishalishaji wa mazao ya chakula nchini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Mwanamvua Mrindoko leo Julai 03,2025 alipokuwa akizungumza na waandishi Wa Habari Jijini Dodoma, ambapo amesema katika kipindi cha Uongozi wa Awamu ya Sita, Mkoa wa Katavi umepokea Jumla ya Kiasi cha Fedha Trilioni 1.345 fedha hizi zikielekezwa katika Kukuza Uchumi, kuboresha na Kustawisha Jamii, Miradi ya Maendeleo, Utawala Bora, uwajibikaji na Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo.
Katika Kuiangazia Sekta ya Elimu, Mkoa wa Katavi Umepokea Jumla Bilioni 58 .093 kwa ambapo jumla ya Shule Mpya 137 zimejengwa, Shule 97 zikiwa ni za Sekondari, na 40 zikiwa ni Shule za Msingi.
.
Kwa Upande wa Shule ya Msingi, jumla ya Madarasa mapya 2219 yamejengwa, Madawati 32,728 yametengenezwa, Matundu ya Choo 2,734 yamechimbwa na jumla ya Nyumba 74 za walimu zimejengwa.
Aidha, Kwa upande wa Shule za Sekondari, madarasa Mapya 559 yamejengwa, Viti na Meza 15213 na Matundu ya Vyoo 2147 yamejengwa.
.
Upande wa Rasilimali watu jumla ya Walimu 555 wameajiliwa kwa ngazi ya Shule za Msingi na 424 wameajiliwa kwa ngazi ya Shule za Sekondari.
Mkoa wa Katavi pia unaendesha miradi miwili ya Ujenzi wa vyuo vya Elimu na Mafunzo Stadi, VETA.
.
Miradi hii inatekelezwa katika wilaya ya Tanganyika na Milele kwa jumla ya kiasi cha Fedha shilingi Bilioni 3.233 na yote inategemea kukamilika katika kipindi cha mwaka huu wa Fedha 2024/2025.
.
Mbali na Hayo, Mkoa unafanya upanuzi wa Chuo Kikuu cha (Sokoine Kampasi ya Mizengo Pinda) ambapo upanuzi huo utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 17.46 mpaka kukamilika.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

