MAWAKILI MSIBANANE MIJINI,NENDENI VIJIJINI MKATATUE MIGOGORO YA WANANCHI -JAJI MKUU MASAJU
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. George Mcheche Masaju amewataka Mawakili wapya wa Kujitegemea kuacha tabia ya kuchagua maeneo ya kufanyia kazi hususani mijini na badala yake waende pia sehemu za vijijini ili wakatatue changamoto za wananchi wanazokabiliana nazo.
.
Jaji Mkuu ameyasema hayo tarehe 03 Julai, 2025 alipokuwa akiwapokea na kuwaapisha waombaji 449, wakiwemo wanaume 252 na wanawake 197, kuwa Mawakili wapya wa Kujitegemea tukio lililofanyika Mtumba jijini Dodoma.
.
"Niwasihi na kuwaonya kuwa sitopenda kabisa kuwaona mnazunguka zunguka mijini mikubwa kama Dar es Salaam na Dodoma muonekane kama vishoka, sambaeni maeneo ya pembezoni mkafanye kazi ya kutenda haki ili kuisaidia jamii, pia sitaki kusikia mnauza utu wenu kwa kupewa rushwa badala ya kutenda haki,"alisisitiza Jaji Mkuu.
Pia Jaji Mkuu Masaju amewaonya mawakili hao kutopokea fedha na kubadili haki ya mtu mwingine na kuipeleka sehemu nyingine kitendo hicho ni kinyume cha maadili ya kazi hiyo, hatopenda kuona wanakiuka maadili hayo.
.
Aidha, Jaji Mkuu amewataka Mawakili hao kuzisoma sheria za Uchaguzi Mkuu,ili kuwasaidia wagombea kutatua migogoro na kesi zitakazofunguliwa katika mahakama mbalimbali nchini wakati wa uchaguzi na kuwasaidia kujaza fomu waliojitokeza kutia nia, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

