TAI–HABARI YASAJILI WAANDISHI WA HABARI ZAIDI YA 2900 NCHINI TANZANIA
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewaasa waandishi wa habari nchini kuwa walinzi wa ukweli, wajenzi wa amani na wachochezi wa uwajibikaji wa kisiasa.
.
Sambamba na kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinabaki kuwa kioo safi cha jamii kisicho na doa la uzushi, chuki au upendeleo na kuendelea kuhimiza maelewano, uvumilivu wa kisiasa, na utamaduni wa kuheshimu tofauti za maoni.
.
Dkt. Biteko ameyasema hayo Julai 09,2025 jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano wa Wadau Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025.
“Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa waandishi wa habari katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi wanabaki salama wao pamoja na mali zao.
.
"Aidha, Serikali, tutaendelea kulisimamia hili kwa nguvu zetu zote. Tutahakikisha kuwa, mnakuwa na mazingira salama, huru na rafiki wakati wote wa majukumu yenu" alisema Dkt. Biteko.
Amesema katika kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 katika jamii kutakuwa na watu wenye mitazamo mbalimbali kulingana na vipaumbele vyao hata hivyo vyombo vya habari vina fursa ya kutoa uelekeo kwa taifa.
“Uchaguzi ni kipindi cha muda mfupi, tumuombe Mungu hata baada ya Uchaguzi tubaki kuwa Taifa moja lenye ustahimilivu na kila mmoja akitoka kwake aende kutafuta mkate arudi nyumbani kwa familia yake kukiwa na amani, sisi kupitia mkutano huu tuungane kuhakikisha Taifa letu linabaki salama. Sekta ya habari ni nyenzo muhimu katika kulinda na kudumisha amani katika kipindi chote cha uchaguzi,” amesisitiza Dkt. Biteko.
.
Pamoja na ufunguzi wa mkutano huo, Dkt. Biteko amezindua rasmi Mfumo wa Kidigiti wa TAI – Habari wa kusajili na kutoa ithibati kwa waandishi wa habari ambao unasimamiwa na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ambapo hadi sasa Bodi hiyo imesajili waandishi wa habari zaidi ya 2900 kupitia mfumo huo ambao unachakata taarifa zote muhimu za mwandishi wa habari na kisha kumpatia mwandishi wa habari kitambulisho cha kidigiti (yaani Digital Press Card).
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

