logo

BENJAMIN MKAPA HOSPITAL YAJIPANGA KUTEKELEZA DIRA YA TAIFA 2025-2050

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof. Abel Makubi amesema kuwa, hospitali hiyo tayari imeshaanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 na ndiyo maana watalaamu wapo nchini Burundi kutoa hayo Matibabu kama sehemu ya Tiba Utalii.

‎"Tumejipanga kuitekeleza Dira hii iliyo zinduliwa leo kwakuwa imegusa sekta ya afya katika mwelekeo(ustawi wa jamii) , katika malengo, nguzo na matarajio katika azima ya kuwa na Taifa lenye Jamii yenye Afya bora. Serikali kupitia BMH tayari inaendelea kuwekeza kuwa kituo cha kuvutia utalii wa matibabu ya ubingwa na ubobezi kwa kutumia teknolojia za kisasa” alisema Prof. Makubi.

‎Ameongeza kuwa BMH inaendelea kufanya tafiti mbalimbali ili kuendelea kuimarisha utoaji wa huduma za matibabu

‎"Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) tunaendelea kufanya tafiti ambazo zinaendelea kuimarisha huduma tunazozitoa na ndani ya miaka 25 ijayo maono yetu ni eneo la BMH na UDOM kuwa sehemu ya Dodoma Medical Tourism City" alisema Prof. Makubi.

‎Aidha, ameshukuru Dira kuliwekea mkazo suala la upatikanaji madawa na vifaa tiba ambapo sasa tukawekeza katika viwanda vyetu vitakavyo zalisha vifaa tiba na vitendanishi.

‎"Hivi karibuni tumeshuhudia Waziri wa Afya wakiingia hati yamakubaliano na shirika moja ambalo litaanza kuzalisha vifaa tiba Tanzania, hii ni hatua ya kupongezwa na inatakiwa kuendelezwa ili tupate mashirika mengi zaidi ya uzalishaji wa vifaa tiba na vitendanishi" alisema Prof. Makubi.

‎Hospitali ya Benjamin Mkapa imewekezwa kwa vifaa tiba kisasa na madaktari Bingwa hali inayopelekea kupeleka huduma nje ya Dodoma na nje ya Tanzania kutokana na uwekezaji wake na hivi sasa kuna timu ya madaktari Bingwa wapo Burundi kutoa huduma.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn