logo

MARA YAVUNJA REKODI UPATIKANAJI WA MAJISAFI NA SALAMA VIJIJINI MWAKA 2020/25

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi amesema hali ya upatikanaji wa maji safi na salama vijijini umeongezeka katika mkoa huo kutoka asilimia 54 mwaka 2021 hadi asilimia 81 Juni, 2025.

‎.

‎"Upatikanaji wa maji safi na salama katika miji unaridhisha na hadi kufikia Juni, 2025 upatikanaji wa maji katika Manispaa ya Musoma ni asilimia 98, Mji wa Mugumu asilimia 67, Mji wa Tarime asilimia 77 na Mji wa Bunda ni asilimia 86" alisema.

‎Kanali Mtambi ameyasema hayo leo Julai 18,2025 alipokuwa akizungumza na Watanzania kupitia mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika mkoa huo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dodoma.

‎.

‎Amesema Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere imeanza kuzalisha gesi tiba ya oksijeni kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wanaohitaji huduma ya gesi tiba pamoja na kuhudumia vituo jirani.

‎.

‎"Uwepo wa hospitali hii pamoja na uboreshaji mkubwa uliofanywa katika vituo vya kutolea huduma za afya umesaidia kupunguza rufaa za wagonjwa kutoka Mkoa wa Mara kwenda Hospitali ya Kanda Bugando kwa asilimia 70" alisema Kanali Mtambi.

‎.

‎Aidha, Kanali Mtambi amesema VETA imejenga vyuo vitano vya ufundi katika Wilaya za Butiama, Rorya, Serengeti, Tarime na Bunda kwa gharama ya shilingi bilioni 12.71.

‎.

‎"Ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya ya Butiama umekamilika na mafunzo yameanza kutolewa na vyuo vinne vingine unaendelea" alisema Kanali Mtambi.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn