logo

BODI YA MFUKO WA BARABARA YAKAGUA KM 223.5 SINGIDA HADI MINJINGU

Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB),wametembelea na kukagua barabara yenye urefu wa kilomita 223.5, ya Singida-Katesh-Dareda-Babati Hadi Minjingu,mkoani Singida.

‎Ziara hiyo imefanyika Septemba 18,2025, mkoani Singida ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Mussa Natty wakiwa wameambatana na wataalamu kutoka Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) Mkoa wa Singida.

‎Ambapo wajumbe wa Bodi hiyo wamekagua hali ya barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 223.5, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya RFB kukagua na kujionea utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara inayofanywa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Barabara.

‎Hata hivyo Singida umekuwa Mkoa wa pili,ukitanguliwa na Mkoa wa Dodoma kwa wajumbe wa bodi hiyo kutembelea,kukagua na kujionea utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara inayofanywa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Barabara.

‎Wakati bodi hiyo ikiwa mkoani Dodoma,ilifanyika Septemba 17,2025 wajumbe waliopata fursa ya kujionea matengenezo ya barabara ya Dodoma hadi Kitinku yenye urefu wa Km 66.7,uliogharimu kiasi cha milioni 911.

‎.

‎Aidha, Bodi ya Mfuko wa Barabara itaendelea na zoezi hilo la ukaguzi katika Mikoa ya Manyara na Arusha, ili kujionea utekelezaji wa miradi ya matengenezo ya barabara inayofanywa kwa fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Barabara.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn