WAANDISHI WA HABARI WAJENGEWA UELEWA JUU YA SHERIA YA ULINZI WA WATOA TAARIFA NA MASHAHIDI JIJINI DODOMA
Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki, imetoa mafunzo ya Sheria ya Watoa Taarifa na Mashahidi, Sura ya 446 kwa Waandishi wa habari na Wahariri kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu sheria hiyo.
Akifungua rasmi kikao kazi hicho Oktoba 27, 2025 Jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Bi, Akisa Mhando amesema kuwa kikao hicho kina lenga kuwaongezea maarifa waandishi wa habari juu ya Sheria ya Ulinzi wa watoa taarifa na Mashahidi.
Amesema kuwa baada ya kikao kazi hicho vyombo vya habari vitakuwa na uwezo wa kuuhabarisha Umma na kuwahamasisha wananchi kuwa tayari kushiriki katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za uhalifu kwa lengo la kujenga jamii yenye Amani, usalama na Utulivu kwa mazingira wezeshi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi na wananchi.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

