WANANCHI WAHIMIZWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU PALE AMBAPO ELIMU YA ULINZI WA WATOA TAARIFA ITAKAPOTOLEWA TANZANIA
Wito umetolewa kwa Wananchi nchini kujitokeza kwa wingi pale ambapo elimu ya Ulinzi kwa watoa taarifa na Mashahidi itakapotolewa katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili waweze kupata ufahamu undani wa elimu hiyo ili tuweze kutokomeza uhalifu nchini.
.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Akisa Mhando, tarehe 28 Mwezi Oktoba,2025 alipokuwa akifunga kikao kazi cha wadau wa Sheria ya Watoa Taarifa na Mashahidi Sura No.446 kilichofanyika siku 2 jijini Dodoma.
.
Amesema lengo kuu la kikao hicho ni kutoa elimu hiyo kwa Wahariri na Waandishi Wa Habari ili nao waweze kutoa elimu hiyo waliyoipata kwa jamii husika,ili waweze kufahamu undani wa sheria hiyo pamoja na kanuni zake husika.
.
Aidha, amesema mpaka hivi sasa kwenye Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki wamefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ikiwemo Wahariri na Waandishi wa habari nchini ambapo kundi hilo limepata uelewa wa sheria hiyo kiundani zaidi.
.
"Na katika uelewa huo, wametuthibitishia wenyewe ya kwamba wamepata somo kubwa juu ya sheria hiyo, na pia tumepanga mikakati mbalimbali na nyenzo zitakazotusaidia katika kufikisha ujumbe wa sheria hii kwa umma" alisema Bi. Akisa.
.
Kikao hicho kiliwakutanisha wataalam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, waandishi wa Habari, Wahariri kutoka katika vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari vya mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwasaidia waandishi kuielewa Sheria ya Ulinzi wa kwa watoa taarifa na Mashahidi ili kuwasaidia kuuelimisha Umma kuhusu umuhimu wa sheria hii.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

