logo

WACHUMBA WAHAIRISHA KUFUNGA NDOA BAADA YA KUKIRI KUZINI

WACHUMBA wawili kutoka Kaunti ya Tana River iliyopo Nchini Kenya wamelazimika kuhairisha sherehe yao ya kufunga ndoa kwa muda wa mwaka mmoja baada ya wao kukiri mbele ya mchungaji wao kuwa wamekua wakishiriki ngono kabla ya kuoana rasmi.

.

Inaelezwa kwamba wakati wa kikao cha ushauri na maungamo kwa wanandoa hao watarajiwa, bwana harusi alikiri lakini bibi harusi mtarajiwa alikana kuwahi kushiriki tendo hali ambayo ilimfanya Mchungaji kuwaita ofisini na baadae kukiri.

.

Hatua hiyo ilimfanya Mchungaji Eli Mwakisha, kukasirika na kutishia kuwalaani wawili hao. Mwakisha aliwafukuza ofisini kwake na kuita timu ya maombezi kwa ajili ya sakata hilo.

Baada ya saa mbili za maombi mazito, aliwaita tena ofisini na kuwaambia watengane na kusimamisha mipango ya harusi kwa muda wa miezi 12 huku akisema hayo yalikuwa ni maagizo ya Mungu.

Kiongozi wa maombi katika kanisa hilo Helida Kase, amesema wawili hao waliagizwa kutumia muda huo kutubu na kuomba, lakini pia wahakikishe wanahudhuria ushauri wa wanandoa kila Jumatano, Ijumaa na Jumapili.

Wanandoa hao watarajiwa walikataa kuzungumzia suala hilo huku baadhi ya waumini wa kanisa wakiona kuwa hio haitakuwa harusi ya kwanza kusimamishwa au kufutwa, kama ilivyo kawaida wakati watarajiwa walio katika uchumba wakigundulika wamefanya mapenzi kabla ya ndoa.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn