BMH YAANDIKA REKODI YA KUONDOA MAUMIVU SUGU YA MGONGO BILA KUFANYA UPASUAJI
Daktari Bingwa wa Ubongo na mishipa ya fahamu Hospitali ya Benjamin Mkapa Maxgama Ndosi ameeleza kuwa matibabu haya ni ya ubingwa wa juu.
"Leo tumeanzisha matibabu haya na tunafanya sisi wenyewe kwa maana ya madaktari Bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, tumefanikiwa kumuhudumia mgonjwa wa kwanza na ametoka salama, matibabu haya yanahusisha sindano maalumu katika uti wa mgongo mgonjwa akishapata matibabu haya maumivu ya mgongo yanaondoka kabisa" alisema Dkt. Ndosi
Ameongeza pia matibabu haya yanaondoa adha ya mgonjwa kukaa wodini
"Matibabu haya ya namuondolea adha mgonjwa kukaa wodini kwa kuwa hayausishi upasuaji, hivyo anapopatiwa matibabu haya anaondoka siku hiyo hiyo "amesema Dkt. Ndosi
Kwa upande wa mgonjwa (jina limehifadhiwa) ameeleza baada ya kupata matibabu hayo
"Nilikuwa namaumivu makali sana ya mgongo ilikuwa inanipelekea kushindwa kutembea au kuinua vitu lakini baada ya kupata matibabu haya nilipo maliza kuchoma sindano hapo hapo sikusikia maumivu mpaka sasa sina maumivu" alisema Mgonjwa
Hospitali ya Benjamin Mkapa inakuwa ni ya pili kutoa matibabu haya nchini na ni ya kwanza kwa ukanda wa kati, wakati Hospitali ya Benjamin Mkapa ikiadhimisha miaka kumi tangu ianze kutoa huduma imeendelea kuongeza huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa wa juu.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

