MPANGO MPYA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA MTOTO WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM
Taasisi ya Thamini Uhai na Doris Mollel Foundation leo, Desemba 01, 2025 jijini Dar es Salaam, zimesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka mitatu kwa ajili ya kuanzisha mpango mahsusi wa kupambana na vifo vinavyoweza kuzuilika vya wajawazito na watoto wachanga nchini Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Doris Mollel Foundation, Bi. Doris Mollel, amesema ushirikiano huo utalenga kuimarisha mifumo ya afya, kuongeza uwezo wa wataalamu wa afya, pamoja na kushinikiza utekelezaji wa sera bora za afya katika ngazi ya kitaifa.
.
"Dhamira kuu ya mpango huo ni kutoa huduma jumuishi na za kiwango cha juu, ili kuhakikisha hakuna mama au mtoto mchanga anayepoteza maisha kwa sababu zinazoweza kuzuilika" alisema Doris.
Aidha, ameishukuru timu zote mbili, akiwemo Bw. Banzi Msumi, Mkurugenzi Mtendaji wa Thamini Uhai, kwa kuendeleza maono ya pamoja ya kuboresha afya ya mama na mtoto nchini.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

