logo

DCEA YAKAMATA KILO 3,799 ZA DAWA ZA KULEVYA MWEZI NOVEMBA,2025

Katika mwezi Novemba 2025, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imefanikisha operesheni kadhaa zilizoleta matokeo makubwa katika mapambano dhidi ya uhalifu wa dawa za kulevya nchini.

‎Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Disemba 03,2025 Jijini Dar Es Salaam, Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, Bw. Aretas Lyimo, amesema Katika operesheni hizo, jumla ya kilo 3,799.22 za dawa za kulevya zimekamatwa, ekari 18 za mashamba ya bangi zimeteketezwa, na mali za wahalifu zenye thamani ya shilingi bilioni 3.304 zimetaifishwa na Serikali, na watuhumiwa 84 wamekamatwa wakihusishwa na biashara hiyo haramu.

‎.

‎Katika hatua nyingine, Kamishna Jenerali Lyimo amesema kuwa, Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imetangaza uamuzi wa kutaifisha mali za watuhumiwa wawili, Saleh Khamis Basleman na Gawar Bachi Fakir, wanaoshtakiwa kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

‎"Mali zilizotaifishwa zinakadiriwa kufikia Tsh. 3,304,000,000/=, ambazo ni pamoja na nyumba, viwanja na magari, Uamuzi huo umetolewa baada ya uchunguzi kubaini kuwa mali hizo zilipatikana kupitia matendo ya kihalifu yanayohusiana na dawa za kulevya.

‎.

‎"Katika operesheni maalumu iliyotekelezwa katika Mkoa wa Rukwa, katika eneo la mpaka wa Kasesya, mamlaka zilimkamata Godwin Andrew (26), mkazi wa Mbalizi mkoani Mbeya, akiwa na dawa za kulevya aina ya skanka zenye uzito wa kilogramu 244.3. Dawa hizo zilikuwa zimefichwa kwa ustadi mkubwa ndani ya spika, mashine za kupooza hewa, mashine za kukatia majani, pamoja na vifaa vya kompyuta (CPU)" alisema Bw. Lyimo.

‎Amesema Vifaa hivyo vilikuwa vinasafirishwa kwa kutumia gari aina ya Iveco Van lenye namba za usajili za Afrika Kusini CN 85 FN GP, mali ya kampuni ya usafirishaji ya Makamua Logistics Limited, ambalo lilikuwa linatoka Afrika Kusini kuelekea Dar es Salaam.

‎Aidha,Katika operesheni nyingine zilizofanyika maeneo mbalimbali nchini, vyombo vya usalama vilifanikiwa kukamata kilogramu 2,041.45 za bangi, kilogramu 1,423.28 za mirungi, na kuteketeza ekari 18 za mashamba ya bangi, jumla ya magari manne na pikipiki 12 vilikamatwa kuhusiana na matukio hayo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn