logo

MABASI YA UMEME KUANZA ZANZIBAR MWEZI FEBRUARI,2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema usafiri wa umma kwa kutumia mabasi ya umeme Zanzibar unatarajiwa kuanza rasmi mwishoni mwa mwezi Februari, 2026, ukianzia Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.

‎.

Dkt. Mwinyi amesema hatua hiyo inalenga kuboresha huduma za usafiri, kupunguza msongamano wa magari barabarani na kuimarisha matumizi ya nishati rafiki kwa mazingira.

‎"Mradi huo unatekelezwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), ambapo Serikali kupitia ZSSF imeingia mkataba na Kampuni ya GRT Limited kwa ajili ya utekelezaji wake. Mabasi hayo yataendeshwa kwa mfumo wa kisasa, yakitumia vituo maalum pamoja na barabara za kawaida" alisema Dkt. Mwinyi.

‎Kwa upande mwingine, amesema Mradi wa mabasi ya umeme utafanyika kwa awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza itaanzia Mkoa wa Mjini Magharibi ikihusisha njia za Uwanja wa Ndege–Malindi pamoja na BuyuChukwaniMnazi MmojaMalindi, Kituo cha Kijangwani kitatumika kama kituo kikuu cha kuunganisha mabasi yote, huku vituo vingine vikiwa ndani ya Uwanja wa Ndege na Bandari ya Malindi.

‎Aidha, Rais Mwinyi amesema mabasi ya umeme yanatarajiwa kuanza kuwasili mapema mwezi Februari, 2026, kabla ya kuanza kutoa huduma rasmi kwa wananchi.

‎.

‎"Mradi huu ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Nane chini ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika kuimarisha maendeleo ya miundombinu na usafiri wa umma Zanzibar" alisema Dkt.Mwinyi.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn