WANAFUNZI 10 WAPATA UFADHILI WA MASOMO SHAHADA YA UZAMILI SAMIA SKOLASHIPU
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza rasmi kutoa ufadhili wa masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani za Sayansi ya Takwimu, Akili Unde (AI) na Sayansi Shirikishi kupitia mpango wa Samia Scholarship Extended (SSE DS/AI+).
Katika awamu ya kwanza, wanafunzi 10 wamepata ufadhili huo na watasoma katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela.
Vilevile, wanafunzi wengine 10 wanatarajiwa kujiunga na masomo hayo katika Indian Institute of Technology Madras Zanzibar Campus.
Akizungumza na waandishi wa habari Februari 25, 2026 jijini Dodoma, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda, amesema Serikali imeamua kuwekeza katika masomo hayo kutokana na mahitaji makubwa ya wataalamu katika sekta ya sayansi na teknolojia nchini.
.
Ameeleza kuwa jumla ya shilingi bilioni 5 zimetengwa kugharamia utekelezaji wa mpango huo.
Prof. Mkenda pia ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuchangia ufadhili wa masomo kupitia mpango wa Samia Scholarship.
Aidha, wanafunzi waliopata ufadhili wa Shahada ya Kwanza kupitia Samia Scholarship wametakiwa kuangalia majina yao kupitia tovuti za Wizara, Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania na Taasisi ya Nelson Mandela.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

