logo

WHO YAITUNUKU TUZO DORIS MOLLEL FOUNDATION GENEVA NCHINI SWITZELAND ‎

Taasisi ya Doris Mollel (DMF) imetunukiwa tuzo ya heshima kutoka World Health Organization (WHO) kwa kutambua mchango wao mkubwa katika kuboresha afya ya mama na mtoto nchini Tanzania.

‎.

‎Tuzo hiyo imekabidhiwa katika makao makuu ya WHO yaliyopo Geneva nchini Switzerland, na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus, ambapo imepokelewa na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Bi. Doris Mollel.

‎.

‎Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Doris Mollel amesema kuwa heshima hiyo ni matokeo ya juhudi za pamoja katika kuimarisha huduma za afya ya mama na mtoto kupitia mbinu bunifu zinazotokana na jamii zenyewe.

‎.

‎Aidha, shirika hilo limeishukuru WHO kwa kutambua mchango wa suluhisho za ndani (locally-led solutions) na juhudi za kijamii ambazo zimeendelea kusaidia kuboresha huduma za afya na maisha ya wananchi.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn