logo

DCEA YAKAMATA KILO 1,983 ZA DAWA ZA KULEVYA MACHI 2026

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema katika operesheni zake za mwezi Machi 2026 imefanikiwa kukamata jumla ya kilogramu 1,983.31 za dawa mbalimbali za kulevya, kilogramu 3,012.5 na lita 17,960 za kemikali bashirifu, vidonge 286 pamoja na chupa 1,001 za dawa tiba zenye asili ya kulevya.

‎.

‎Hayo yamesemwa na Kamishna Jenerali wa DCEA, Bw. Aretas Lyimo, leo Aprili 13,2026 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya operesheni hizo jijini Dar es Salaam.

‎.

‎Sambamba na ukamataji huo, amesema ekari 55.5 za mashamba ya bangi ziliteketezwa na watuhumiwa 77 kukamatwa kuhusiana na makosa hayo.

‎.

‎"Vilevile, vyombo vya usafiri vilivyotumika kusafirisha dawa hizo vilikamatwa vikiwemo magari tisa, pikipiki 12 na bajaji moja,

‎Uchambuzi wa takwimu umeonesha ongezeko kubwa la ukamataji wa mirungi, ambapo kilogramu 1,267.12 zilikamatwa, sawa na asilimia 64 ya dawa zote zilizokamatwa mwezi huo.

‎.

‎"Ongezeko hilo limetokana na mkakati wa DCEA kujikita zaidi katika operesheni za mashambani baada ya kudhibiti kwa kiwango kikubwa mitandao ya dawa za viwandani" alisema Lyimo.

‎.

‎Amesema katika tukio la jijini Dar es Salaam eneo la Tegeta Kibo, kilogramu 101.2 za mirungi zilikamatwa zikiwa zimefichwa ndani ya basi la abiria aina ya Yutong la kampuni ya Abood Bus Service lenye namba T 181 EMJ, lililokuwa likisafiri kati ya Mombasa, Kenya na Dar es Salaam.

‎.

‎"Dawa hizo zilifichwa hadi kwenye mfumo wa hewa (AC) wa basi hilo ili kukwepa kugundulika. Watuhumiwa waliokamatwa ni dereva Ramadhan Mohamed (52), kondakta Salma Sanga (26), Twahilu Athuman (38), Mohamedy Mikidadi (37) na Ibrahim Mohamed (39)" alisem.

‎.

‎Aidha, wilayani Misungwi mkoani Mwanza kilogramu 184.9 za mirungi zilikamatwa nyumbani kwa Chrispin Shoo (62) na mkewe Esther Pastory (55), pamoja na vyombo vya usafiri walivyokuwa wakivitumia.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn