logo

WAHAMIAJI HARAMU 63 WAKAMATWA KEKO MWANGA, JIJINI DAR ES SALAAM

‎Jumla ya wahamiaji haramu 63 wamekamatwa katika mtaa wa Keko Mwanga, kata ya Keko Mwanga, wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, kufuatia msako maalum uliofanyika alfajiri ya tarehe 13 Aprili 2026.

‎Msako huo uliofanywa na Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam uliongozwa na Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Temeke, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Wilson Ringo, ukiwa na lengo la kudhibiti uwepo wa wahamiaji haramu katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam.

‎Akizungumza na umma kuhusu tukio hilo, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji (SACI) Vicent Haule, amesema operesheni hiyo imezaa matokeo chanya na ni sehemu ya jitihada zinazoendelea za kuimarisha usalama na utawala wa sheria.

SACI Haule amewataka wananchi kuendelea kushirikiana na Idara ya Uhamiaji kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati, ili kusaidia kukomesha tatizo la wahamiaji haramu katika mkoa huo.

‎Amesisitiza kuwa ushirikiano wa jamii ni muhimu katika kuhakikisha udhibiti wa uhamiaji haramu na kudumisha amani na usalama wa eneo la Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn