logo

PROF.MKENDA AKUTANA NA MABALOZI WATEULE,ELIMU KUWEKWA AGENDA YA KIMKAKATI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda leo Aprili 14, 2026 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wateule watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali walizopangiwa.

‎Katika kikao hicho wamekubalina kuwa elimu, sayansi na teknolojia zitakuwa moja ya agenda za kufanyia kazi ikiwemo suala la umataifishaji elimu.

‎Mabalozi wateule wameipongeza Wizara kwa mageuzi makubwa ya elimu yanayoendelea kutekelezwa na kuahidi kuichukua agenda ya elimu kuwa ya kimkakati kwa maendeleo ya taifa.

‎Mabalozi hao ni watakaoiwakilisha Tanzania Saudi Arabia, Zambia, Muscat

‎Comoros, Korea Kusini, Sweden na Umoja wa Mataifa, New York wakiongozwa na Mhe. Balozi Mhandisi Zena Said

‎Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Wizara hiyo.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn