Top news
TANESCO YASAINI MKATABA WA KWANZA UZALISHAJI UMEME JUA
WIZARA ya Nishati kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imesaini mkataba wa kwanza wa uzalishaji wa umeme Jua wa kiasi cha megawati 50 utakaotekelezwa wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Mkataba huo umesainiwa tarehe 29 Mei, 2023 jijini Dodoma na kushuhudiwa na Waziri wa Nishati, Mhe.January Makamba ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Kwa ujumla mradi huo wa umeme wa Jua ni wa megawati 150 ambapo awamu kwanza itajengwa mitambo itakayozalisha megawati 50 na awamu ya pili itajengwa mitambo ya megawati 100 kwa jumla ya shilingi bilioni 275. Utekelezaji wa mradi wa Awamu ya kwanza hautazidi miezi 12.
Akizungumza katika hafla hiyo, Makamba Amesema kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi tunaingiza umeme wa Jua katika gridi ya Taifa.
.
"Nimpomgeze Rais wetu kwa kwa muongozo na uongozi ambao umepelekea nchi kuaminiwa na washirika wa maendeleo ikiwemo Shirika la Maendeleo la Ufaransa ambalo limetoa mkopo ambao utatekeleza mradi huu" Amesema Makamba.
.
Nae Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo Amesema Mradi Huo utakwenda Kutengeneza Fursa ya Ajira Kwa Wananchi Wa Mkoa Wa Shinyanga Hususani Katika Jimbo la Kishapu, Na pia Utakwenda Kuondoa Tatizo la Kukatika Kwa Umeme mara Kwa Mara Katika Mkoa Huo na Mikoa Jirani pia.
.
"Naomba Nitoe Rai Yangu Kwa Wana Shinyanga, Tunaomba muupokee Mradi Huu Kwa Mikono Miwili Ili Uweze kutunufaisha Sisi Wenyewe na Taifa Kwa Ujumla" Amesema Butondo.
@wizara_ya_nishati_tanzania
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

