logo

WANAFUNZI 315,307 WADAHILIWA ‎ELIMU YA UFUNDI MWAKA 2026

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amesema Serikali imeendelea kupanua kwa kasi elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ili kujenga nguvu kazi yenye ujuzi na kuongeza ajira kwa vijana.

‎.

‎Akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkenda amesema udahili umeongezeka kutoka wanafunzi 265,000 mwaka 2025 hadi kufikia wanafunzi 315,307 mwaka 2026.

‎.

‎Amesema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa idadi ya vyuo vya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi kutoka vyuo 1,414 mwaka 2025 hadi kufikia vyuo 1,446 mwaka 2026, ambapo vyuo vya elimu ya ufundi vimeongezeka hadi 532 na vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi kufikia 914.

‎.

‎Katika kuimarisha miundombinu, Serikali imeendelea na ujenzi na ukarabati wa vyuo, ikiwemo ujenzi wa vyuo 64 vya VETA ngazi ya wilaya na chuo kimoja cha ngazi ya mkoa katika Mkoa wa Songwe Region, ambapo wastani wa utekelezaji umefikia asilimia 68.

‎.

‎Aidha, kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Serikali imewezesha ujenzi wa maabara za TEHAMA katika shule 10 za sekondari pamoja na kuvipatia vyuo vifaa vya TEHAMA ikiwemo kompyuta za mezani 213 na kompyuta mpakato 24 ili kuwajengea wanafunzi uwezo wa kutumia teknolojia katika maisha na ajira za kila siku.

‎.

‎Waziri Mkenda amesema uwekezaji huo unaongeza ubora wa ujifunzaji, kuimarisha miundombinu ya vyuo na kupanua fursa za elimu ya amali nchini.

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn