NBAA YAPONGEZWA KWA KUENDELEZA TAALUMA YA UKAGUZI
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Bw.Charles E. Kichere,amesema mabadiliko ya viwango vya kitaaluma na kuongeza kwa matarajio ya wadau ni muhimu kwa wakaguzi kuendelea kujifunza,kujiongezea uwezo na kuendana na mabadiliko hayo ili kuongeza ufanisi,weledi na ubora wa kazi zao.
.
Amewataka Watumishi wote wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (Wahasibu na Wakaguzi) kushiriki mafunzo hayo na pia wasisahau ya kwamba wana wajibu wa kupata CPA.
.
CAG Kichere ameyasema hayo leo Mei 11,2026 jijini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa watumishi wa ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kote nchini.
.
Amesema kama Wakaguzi wanapaswa kuwa na hatua nyingi mbele katika uelewa wa viwango,mifumo na masuala ya kitaaluma ili waweze kutekeleza yao kwa ufanisi na kutoa mwongozo sahihi kwa wakaguliwa.
.
Kwa upande mwingine, CAG Kichere ametoa shukrani za dhati kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) kwa kuendelea kushirikiana kwa karibu na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) katika kuendeleza taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi hapa nchini.
.
"Ushirikiano huu una mchango mkubwa katika kujenga uwezo wa Watumishi wetu na kuhakikisha tunaendelea kwenda sambamba na mabadiliko ya kitaaluma na kiteknolojia yanayotokea duniani kwa ujumla wake" alisema CAG Kichere.
.
Aidha, CAG Kichere amesema NAOT ina matarajio makubwa kupitia mafunzo hayo kwani yataendelea kuongeza uwezo wa Watumishi wao katika kutekeleza majukumu yao kwa weledi,ufanisi na kwa kuzingatia viwango vya kitaaluma vinavyotakiwa.
.
Kwa mwaka huu 2026, Mafunzo hayo yanafanyika kwa mfumo wa HYBRID unaojumuisha mafunzo kwa njia ya mtandao na mafunzo ya ana kwa ana.
.
"Mfumo huu unawezesha Watumishi wengi zaidi kushiriki mafunzo haya kwa ufanisi na urahisi zaidi,awamu ya kwanza washiriki walijifunza mada mbalimbali muhimu na zenye umuhimu mkubwa kwa taaluma ya Ukaguzi ikiwemo matumizi ya mifumo ya taarifa katika ukaguzi wa fedha,masuala ya utawala bora na ufanisi,manunuzi ya umma,maadili na mwenendo wa taaluma pamoja na ukaguzi wa taarifa za uendelevu na mwenendo wake duniani". alisema.
.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

