BoT YASISITIZA MATUMIZI YA MIFUMO YA KIDIJITALI KUPUNGUZA HATARI ZA FEDHA
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba amewataka wataalamu wa fedha na ukaguzi nchini kuongeza kasi ya matumizi ya mifumo ya kidijitali katika miamala ya kifedha ili kupunguza utegemezi wa fedha taslimu na kuimarisha usalama wa sekta ya fedha.
.
Gavana Tutuba ameyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye Semina ya pamoja ya wataalamu wa Uhasibu na Ukaguzi iliyoandaliwa na NBAA pamoja na BoT jijini Arusha.
.
"Matumizi ya teknolojia yataisaidia Tanzania kudhibiti uvujaji wa fedha, kuongeza uwazi wa miamala na kukabiliana na vihatarishi vinavyojitokeza kwenye sekta ya fedha" alisema Tutuba.
.
Aidha, amesema licha ya changamoto za uchumi wa dunia, Tanzania imeendelea kuwa na uchumi imara kutokana na usimamizi mzuri wa sekta ya fedha pamoja na utekelezaji wa mifumo endelevu inayozingatia viwango vya kimataifa.
.
Tutuba pia amesisitiza umuhimu wa kuzingatia masuala ya mazingira, mabadiliko ya tabianchi na utawala bora katika mifumo ya kifedha, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia Taifa kufikia dira ya uchumi wa trilioni moja.
.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi amesema mafunzo hayo yatawajengea uwezo wataalamu katika matumizi ya TEHAMA kwenye sekta ya fedha ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani.
.
Mafunzo hayo yanalenga kuimarisha mfumo wa fedha endelevu kwa kutumia teknolojia sambamba na kuzingatia misingi ya mazingira, kijamii na utawala bora katika sekta ya fedha nchini.
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

