WAZIRI KAIRUKI AWATAKA WAKANDARASI KUZINGATIA MASHARTI YA MIKATABA
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Angellah J. Kairuki amewataka Wakandarasi wanaokwenda Kusimamia Mradi wa Uendelezaji wa Mkoa wa Dar es Salaam awamu ya pili (DMDP 2) unaotarajiwa kuanza kutekelezwa Aprili 2024 kuzingatia masharti ya mikataba yao na wasiwe kikwazo kwenye utekelezaji wa mradi huo.
.
Kairuki Ameyasema Hayo Leo Mei 30,2023 Alipokuwa Akishuhudia utiaji saini wa mikataba ya kusanifu Mradi huo Ambao utagharimu Shilingi Bilioni 800.
.
Amesema ofisi yake itahakikisha utekelezaji huo unakuwa na mafanikio makubwa na kuonya dosari zilizojitokeza kwenye awamu iliyopita zisijirudie.
“Mradi huu unakwenda kutatua kero mbalimbali ikiwamo ujenzi holela wa makazi, miundombinu duni ya usafiri, mabadiliko ya tabia nchi kwa jiji la Dar es Salaam zinazosababisha mafuriko na utupaji taka ngumu ovyo.
“Wabunge wa maeneo husika hakikisheni mnasimamia halmashauri zenu ili utekelezaji wa mradi huu uwe na mafanikio na kusiwepo dosari, TAMISEMI tutakuwa makini kuhakikisha kwamba mradi huu awamu ya pili unatekelelezwa kwa mafanikio makubwa, tunaamini tutakuwa tumejifunza kupitia utekelezaji wa awamu ya kwanza,”amesema Kairuki.
Kwa Upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema mradi huo ulikuwa kilio kikubwa kwa wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam ambao kila bajeti walikuwa wakisimama kuhoji.
Awali, akitoa maelezo ya mradi huo, Mratibu wa miradi ya serikali kupitia mikopo ya Benki ya Dunia, Tamisemi na Tarura, Mhandisi Humphrey Kanyenye, amesema asilimia 74 ya fedha hizo zitatumika kwenye miundombinu ya barabara, mifereji, maeneo ya wazi, masoko, vituo vya mabasi, kurekebisha miundombinu ya taka ngumu.
.
Mikataba hiyo imesainiwa kati ya Ofisi hiyo na Wakandarasi wanaosanifu mradi huo ambao ni Mhandisi Consultancy LTD & Luphan (Halmashauri ya Temeke na Kigamboni), Nimeta Consultancy LTD (Halmashauri ya Kinondoni na Ubungo) na UWP Consultancy LTD(Halmashauri ya Dar es Salaam).
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

