logo

WAZIRI MAKAMBA AMESEMA VITONGOJI 2,034 NCHINI BADO HAVIJAFIKIWA NA UMEME

WAZIRI wa Nishati Mhe.January Makamba Amesema Bado asilimia zaidi ya 50 ya vitongoji nchini havijafikiwa na umeme, kazi zilizopangwa kutekelezwa kwa mwaka 2023/24 ni pamoja na, ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme katika vitongoji 2,034 nchini ambavyo bado havijafikiwa na miundombinu ya umeme.

.

"Kwa kuanzia, REA imetenga jumla ya shilingi bilioni 377.05 fedha za ndani kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu"

.

Makamba Ameyasema Hayo Leo Mei 31,2023 Alipokuwa Bungeni Jijini Dodoma Akiwasilisha Bajeti Ya Makadirio Ya Mapato Na Matumizi ya Wizara Hiyo Kwa Mwaka Wa Fedha 2023/24.

.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati, inaandaa Mpango Maalumu wa kupeleka umeme katika vitongoji vyote nchini ndani ya miaka mitano badala ya takribani miaka 20 kwa utaratibu wa sasa.

.

"Kwa sasa zoezi la uchambuzi wa namna ya ugharamiaji wa azma hiyo, ikiwemo kupitia ushiriki wa Sekta Binafsi linaendelea" Amesema Makamba.

.

Aidha, Makamba Amesema uzalishaji wa gesi asilia umeongezeka hadi kufikia Futi za Ujazo bilioni 68.02 ikilinganishwa na Futi za Ujazo bilioni 59.96 kwa kipindi kama hicho mwaka 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 13.

.

"Ongezeko hilo limetokana na hatua zilizochukuliwa za ukarabati wa visima vya uzalishaji wa gesi asilia" Amesema Makamba.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn