logo

BWAWA LA MAJI KIDUNDA UJENZI WAKE UTAANZA MWEZI JUNI 2023

WAZIRI wa Maji Mhe. Jumaa Aweso Amesema Maandalizi muhimu ya usanifu yanaendelea hata kabla ya tarehe rasmi ya kuanza mradi huo kwani mkataba huo unahusisha Usanifu na Ujenzi wa Mradi.

.

Aweso Amesema hadi sasa kazi muhimu za maandalizi ikiwa ni pamoja na kupima sampuli za udongo, kujua uhimilivu wa miamba, nguvu za maji mtoni zimekamilika na kuonesha matokeo chanya.

.

Aidha, Waziri Huyo Amesema mkandarasi pia ameanza ujenzi wa kambi rasmi ya mradi, kambi ya vijana watakaoshiriki ujenzi na uandaaji wa vifaa na mitambo.

.

"Pia; utekezaji wa mradi huo wa kihistoria mbali na kuhifadhi maji lita billion 190, utasaidia pia kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 20" Amesema Aweso.

@jumaa_aweso

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn