logo

WAZIRI KAIRUKI AMESEMA MAOMBI YA KAZI YALIYOPOKELEWA KWENYE MFUMO NI 171,916

WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Angellah Kairuki leo Juni 5, 2023 amebainisha idadi ya watu waliowasilisha maombi ya kazi katika kada ya Ualimu na Afya kupitia mfumo wa kielektroniki wa kupokea na kuchakata maombi ya ajira yaliyoanza rasmi tarehe 12/04/2023 hadi 25/04/2023

Kairuki amesema, jumla ya maombi 171,916 yakiwemo ya wanawake 76,190 na Wanaume 95,726 yamepokelewa kwenye mfumo, na katika maombi ya Kada za Afya yalikuwa ni 48,705 na Kada ya Ualimu ni 123,211.

Ameongeza kuwa ofisi ya Rais iliunda Timu Maalumu ya Uchambuzi ambayo ilifanya kazi ya kuchambua na kuhakiki maombi mbalimbali ya ajira, uhakiki ambao umefanyika katika hatua mbalimbali na kutokana na idadi ya waombaji kuwa kubwa, timu ya Uchambuzi wa Maombi ya Ajira ilipewa vigezo vya kuzingatia ambavyo ni pamoja na mwaka wa kuhitimu na Umri wa kuzaliwa.

Ikumbukwe mnamo Aprili, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa kibali cha ajira ya watumishi 21,200 huku kati yao 13,130 walikuwa wa kada ya Ualimu na 8,070 wa kada za Afya mwezi.

Cc:@kwanzaproduction

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn