logo

CWT HALI TETE, KAMATI YA TENDAJI YAMTAKA KATIBU MKUU KUTOJIHUSISHA NA SHUGHULI ZA CHAMA

KAMATI ya Utendaji ya Taifa ya Chama Cha Walimu Tanzania CWT imemsimamisha Kiutendaji Katibu Mkuu Wa Chama Hicho Josephat Maganga, Kwa Tuhuma za Uvunjifu Wa Katiba Ya Chama Hicho na Kanuni zake Ikiwemo Matumizi Mabaya ya Madaraka na Fedha.

.

Akizungumza na Waandishi Wa Habari Jijini Dodoma Jana Juni 6,2023 Mwenyekiti Wa Kikao Cha Kamati ya Utendaji Taifa ya Chama Cha Walimu Tanzania Mwl.Thobias Sanga ambaye Ni Mwakilishi wa Walimu Kutoka Njombe, Alisema Kuna Changamoto Kubwa Katika Utendaji Hasa Matumizi ya 2% Makato ya Mshahara Wa Walimu.

.

Kikao Hicho kimefanyika Chini Ya Mti kikiwa na Wajumbe 18 Kati Ya 32 Wa Kamati Ya Utendaji ya Taifa ya CWT, wakimsimamisha Kiutendaji Katibu Mkuu Wa Chama Hicho Hadi pale Tuhuma Zake zitakapofikishwa Katika Baraza Kuu.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn