logo

SHINYANGA YAAHIDI USHIRIKIANO KATIKA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameiahidi Wizara ya Katiba na Sheria na wadau inayoshirikiana nayo katika kuendesha kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria Mama Samia Legal Aid Campaign kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kufikia malengo ya kampeni hii ya kutoa msaada wa kisheria kwa watanzania wote hasa wale waishio maeneo ya pembezoni huku akiagiza kata zote zihakikishe zinanatenga maeneo maalum ambayo watoa huduma wataweza kuongea na mwananchi mmoja mmoja kwa faragha.

.

Mndeme ametoa kauli hiyo alipokuwa akihutubia kabla ya kuzindua rasmi utekelezaji wa kampeni hiyo mkoani Shinyanga hafla iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba Shinyanga mjini leo Juni 06,2023

.

huku akiwaalika wakazi wote wa mkoa wa Shinyanga kushiriki Mama Samia Legal Aid Campaign itakayotolewa bure kwa wanachi katika Halmashauri zote sita kuanzia tarehe 11 - 21 Juni, 2023.

.

“Kwa mara nyingine tena, ninatoa wito kwamba sisi sote tushikamane katika kumuunga mkono Kiongozi wetu, Mama yetu, Mlezi wetu na Mtetezi wa Wananchi hususan wanyonge Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania katika kuondoa kadhia na viashiria vyote vya kuminya upatikanaji wa haki hususan ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake na Watoto ambayo ndiyo changamoto kubwa ya Mkoa wa Shinyanga”.Alisema Mndeme.

.

Mkuu Huyo aliongeza kuwa kampeni hiyo inakumbusha watanzania wote uwajibikaji na usimamizi wa maamuzi yenye kuleta haki na akatumia fursa hiyo kuwambusha watumishi wote kutojihusisha na masuala ya rushwa inayopelekea kuzorotesha upatikanaji haki.

.

Aidha, Mndeme amemuahidi Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa katika utekelezwaji wa Kampeni hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu, ofisi yake itasimamia maadili kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa haki kwa usawa.

.

Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria Mhe.Pauline Gekul amesema Wizara itaendelea kushirikiana na Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar kuhakikisha Kampeni hiyo inatekelezwa ipasavyo ili kuwafikia watanzania kwenye Kata na Mitaa yote nchini.

.

Kwa Upande Wake Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi.Mary Makondo ametaja mafanikio ya kampeni hii toka ilipozinduliwa Mkoani Dodoma na kuendelea katika mkoa wa Manyara kuwa ni pamoja na kusuluhishwa kwa migogoro mingi ya kijamii na hata kifamilia iliyohusu ardhi iliyodumu miaka minne, mitano, na mwingine miaka kumi kulikopelekea watu hawa ambao walikuwa hawasalimiani na hata hawazikani kumaliza tofauti zao.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn