PANGANI YAPANGA KUJA NA 'BODA BODA SACCOS'
MKUU Wa Wilaya Ya Pangani Mhe. Zainab Abdallah (@zainababdallah93) Leo April 19,2023 Ameshiriki Mkutano Mkuu wa Bodaboda wilaya ya Pangani Ambao ulikuwa Na Kauli Mbiu isemayo “Uchumi, Uongozi na Maadili.”
.
Katika Kikao Hicho, Zainab amesema Wamekubaliana kuunda SACCOS ya bodaboda ambapo Yeye Binafsi Atawachangia Shiling Milioni 5, Na Mbunge Wa Jimbo la Pangani Mhe. Jumaa Aweso (@jumaa_aweso) Amefanya Harambee na kuchangia Shiling Milioni 65.
.
Mkuu Huyo Amesema kupitia michango yao binafsi wana uwezo wa kukusanya Zaidi ya Shiling Milioni 30 kwa Mwezi huku Lengo ni kuhakikisha kila kijana anaweza Kumiliki BodaBoda yake.
.
"Tunaahidi kushirikiana na taasisi zote za kifedha kuhakikisha azma hii inafikiwa" Amesema Zainab.
#JordanMediaupdates
Tranding News
Newsletter
Subscribe to our newsletter to get the latest news

