logo

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NA USTAWI WA JAMII WATAKIWA KUZINGATIA MAFUNZO YA 'MMMAM'

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake Na Makundi Maalum Mhe.Mwanaidi Ali Khamis Amewataka Maafisa Maendeleo Ya Jamii Na Ustawi wa Jamii wanaoshiriki Mafunzo ya Kitaifa Ya Sayansi Ya Malezi, Makuzi Na Maendeleo ya Awali Ya Mtoto (MMMAM)Kuzingatia Mafunzo Hayo Ili Lengo la Kupata Wataalamu Wenye Weledi Kuhusu Sayansi Na Malezi na Makuzi ya Maendeleo ya Awali ya Mtoto lifikiwe Kwa Urahisi.

.

Mwanaidi Ameyasema Hayo Leo Juni 26,2023 Jijini Dodoma Alipokuwa Akifungua Mafunzo ya Kitaifa Ya Sayansi Ya Malezi, Makuzi Na Maendeleo ya Awali Ya Mtoto (MMMAM) Katika Ukumbi Wa St.Gaspel Hotel.

.

Mwanaidi Amewataka Maafisa Hao wanapotoka kwenye Mafunzo Hayo wawe Mabalozi Kwa Watu Ambao Hawana Uelewa Juu ya Malezi Kwa Watoto.

.

"Mafunzo Haya yasiishe Hapa Tu Bali Muyapeleke Hadi Vijijini Kwa Sababu huko ndio Sehemu Penye Shida Ya Malezi na Makuzi maana wao wanachelewa kupata Taarifa kama Hizi ambazo zinatoka kwenye Serikali Sio Wengi Wenye Vyombo Vya Habari" Alisema Mwanaidi.

.

Naibu Waziri Huyo Amesema Maafisa Hao wanapaswa Kuwa Mabalozi Wa Kutosha Kwa Dhana ya Malezi na Makuzi Jumuishi Ya Watoto wadogo Wenye Kuzingatia Afya Bora, Lishe Ya Kutosha, Ujifunzaji Na Uchangamshaji Wa Awali.

.

Aidha, Mwanaidi Amewataka Maafisa Hao wanapotoka kwenye Mafunzo Hayo wawe Mabalozi Kwa Watu Ambao Hawana Uelewa Juu ya Malezi Kwa Watoto.

.

Nae Mwakilishi Wa Mkurugenzi Wa Shirika la Children in Cross Fire Bw. Frank Samson Amesema Fursa Tuliyonayo ya Kuwa na Takribani Asilimia 26 ya Watoto Wenye Umri Kati Ya Miaka 0 Hadi 8 kulingana Na Sensa Ya Mwaka Uliopita 2022 inawapa Fursa Kubwa ya Kuandaa Taifa tunalolitaka linalokuja.

.

Aidha, Samson Amesema Mafunzo Hayo Ni Ya Muhimu Sana Katika Kuandaa Rasilimali Watu Ambayo yatasaidia Sana Kujenga Taifa Lenye Tija Kwa Siku za Usoni.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn