logo

WAZIRI AWESO AITAKA BODI MPYA MFUKO WA TAIFA WA MAJI NA BODI YA WAKURUGENZI RUWASA KUTOKUFANYA KAZI KWA MAZOEA

WAZIRI Wa Maji Mhe.Jumaa Aweso Amewataka Watendaji Wa Mfuko Wa Maji Wa Taifa Kubadilika Kiutendaji na Kutokufanya Kazi Kwa Mazoea, na Badala Yake watumie Teknolojia Kwa Ajili ya Kufanya Mageuzi Na Urahisishaji Wa Utendaji Katika Kazi.

.

"Lazima Tuangalie Mifuko Mingine wanafanyaje Kazi Kwa Mfano: Mfuko Wa Barabara wanafanyaje. Tubadilike Tusifanye Kazi Blind".

.

Aweso Ameyasema Hayo Leo Juni 27,2023 Alipokuwa Akizindua Bodi Ya Mfuko Wa Taifa Wa Maji Na Bodi Ya Wakurugenzi ya Wakala Wa Maji Na Usafi Wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Katika Ukumbi Wa PSSF Jijini Dodoma.

.

Amesema Mfuko Wa Maji Ni kichocheo Kikubwa Sana Juu ya Utekelezaji Wa Miradi Ya Maji Hivyo Ameitaka Bodi Hiyo Kwenda Kutengeneza Vyanzo Vingine Vya Mapato Ili kuweza Kujiendesha Wenyewe na Kutokutegemea Zaidi Fedha Ya Serikali.

.

"Tunamshukuru Sana Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Hakuna Hata Mwezi Mmoja Hatupati Fedha. Isiishie Tu Hii Fedha ambayo tunayoipata Ya Serikali Ebu tuangalie Sasa Tukatengeneze Vyanzo Vingine Vya Mapato.

.

"Mbona Kuna Asasi Za Kiraia (NGO'S) zinapata Fedha na zinafanya Kazi Vizuri kwenye Miradi ya Maji. Huu Mfuko Ebu Tuangalie Na Tunaweza tukawaomba Wadau Mbalimbali tuone Namna Gani ya Kuweza Kuongezea Lakini Chanzo Chake Kimebaki Hicho hicho" Amesema Aweso.

.

Aidha, Waziri Huyo Amewasisitiza Watumishi hao Kila Anatakiwa Kufanya Kazi Kwenye Nafasi yake Ili Kuhakikisha Mfuko Huo Haukwami Katika Kutekeleza Majukumu yake.

.

Nae Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo Mhandisi.Nadhifa Kemikimba Amesema Kwenye Eneo la Usafi Wa Mazingira Bado hakuna Ripoti yoyote Ya Utendaji mzuri Wa Kazi hivyo Bodi Hiyo Mpya Ya RUWASA iliyozinduliwa inapaswa kwenda Kufanya Kazi zaidi kwenye Sehemu hiyo.

.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti Wa Bodi Hiyo Mpya Ya RUWASA Mhandisi.Ruth Koya Amemuahidi Waziri Aweso atatumia uweledi na Uzoefu aliyokuwa Nao kuiongoza RUWASA Ili kuweza Kufikia Malengo Husika.

#JordanMediaupdates

Frank Jordan
12345 123
Follow Us
logo

© 2023 Jordan Media. All Rights Reserved. Designed by Lylical Popcorn